Motsepe ana imani na Kenya kuandaa AFCON mwaka ujao

Waziri wa Michezo Salim Mvurya, alitoa hakikisho la Kenya kujitolea na kukamilisha ujenzi wa viwanja kwa wakati ufaao.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kinara wa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) Patrice Motsepe ana imani na Kenya,Uganda na Tanzania kuwa tayari kwa wakati ufaao, ili kaundaa fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwaka ujao AFCON.

Motsepe alisema haya Ijumaa baada ya kukagua ukarabati unaoendelea katika uwanja wa Kasarani na ujenzi wa uga wa Talanta katika kaunti ya Nairobi.

Hata hivyo Motsepe alitaka marekebisho kadhaa kufanywa ili kuafiki viwango vya kimataifa.

Alielezea matumaini yake ya viwanja vhivyo viwili kukamilika kufikia Januari mwaka ujao wakati atarejea kwa ukaguzi wa mwisho.

Akiwa Dar es Salaam Alhamisi wiki hii, baada ya kukagua uwanja wa Benjamin Mkapa ,Motsepe aliondolea mbali uwezekano wa mashindano hayo kuhamishiwa kwingine.

Waziri wa Michezo Salim Mvurya, alitoa hakikisho la Kenya kujitolea na kukamilisha ujenzi wa viwanja kwa wakati ufaao.

Kenya,Uganda na Tanzania zitaandaa kwa pamoja makala ya 36 ya patashika ya AFCON kati ya Juni 19 na Julai 17 mwaka ujao.

 

Share This Article