Mirriam Cherop wa Kenya amenyakua nishani ya shaba katika mbio za maili moja kwa wanawake mapema Jumamaso katika mashindano ya Dunia ya mbio za barabarani mjini Copenhagen,Denmark.
Cherop alimaliza wa tatu akiweka muda bora wa msimu wa dakika 4 sekunde 25.71.
Agatha Guillemot wa Ufaransa alkishinda dhahabu kw akutumia dakika 4 sekunde 22.74,huku fedha ikimwendea Mwethiopia Freyweni Hailu kwa dakika 4 sekunde 25.35.
Naomi Korir pia wa Kenya alichukua nafasi ya nne.

Hata hivyo,mambo yalikuwa magumu kwa wanaume Brian Komen, akimaliza wa 14 huku Kyumbe Munguti akiridhia nafasi ya 25.
Mbio hizo zilishindwa na Robert Farken wa Ujerumani,naye Yared Nuguse wa Marekani akanyakua fedha kisha shaba ikamwendea Reuben Querilinjean wa Luxemborg.