Atlas Lions ya Morocco wakicheza nyumbani mjini Rabat, walianza vyema mechi za kufuzu kombe la Afrika mwaka ujao baada ya kuwashinda Gabon mabao 2-0, katika mchuano wa kundi A wa kufuzu uliosakatwa Ijumaa usiku mjini Rabat.
Noussair Mazraoui na Soufiane Rahimi, walipachika bao moja kila mmoja katika kila kipindi na kuwahakikishia Simba wa Atlas ushindi.
Katika mechi nyingine ya kundi hilo Niger waliibwaga Lesotho 2-1.
Kundini B Malawi waliilaza Sudan Kusini 2-1,nao Misri wakalazimishwa sare tasa na Palancas Negras ya Angola.
Dessert Foxes ya Algeria walipata ushindi wa 3-1, dhidi ya Zam,bia katika kundi I,wakati Togo, wakiilemea Burundi moja bila mjini Lome, katika pambano jingine la kundi hilo.
Sudan iliwalemea Ethiopia bao moja nunge katika kundi J,huku Simba wa Teranga kutoka Senegal, wakilazimishwa kwenda sare ya 1-1 na Msumbiji mjini Maputo.
Rwanda wakicheza nyumbani waliinyuka Liberia 3-1,nao Mali wakiititiga Cape Verde pia tatu moja katika mechi za kundi K.
Taifa Stars ya Tanzania ilizimwa nyumbani mabao 2-0 na Guinea Bissau katika kundi L, wakati Nigeria Super Eagles wakitoka nyuma bao moja na kuwalemea Madagascar 2-1 .