Marekani wajaa raundi ya 32 bora ya Kombe la Dunia

Ni mara ya nne mtawalia kwa Marekani kufuzu kwa raundi ya mwondoano ya Kombe la Dunia.

Dismas Otuke
1 Min Read

Waandalizi wenza wa Kombe la Dunia mwaka huu Marekani almaarufu The Stars and Stripes, ndiyo timu ya pili kufuzu kwa awamu ya 32 bora baada ya kuwacharaza Australia, mabao mawili kwa nunge katika mechi hya kundi D iliyopigwa Ijumaa usiku uwanjani Seatle.

Marekani wanaofunzwa na Mauricio Pochettino walijipata uongozini kupitia kwa bao la dakika ya 11, alilojifunga Cameron Burgess.

Alex Freeman alikamilisha kibarua kwa goli la pili dakika mbili kabla ya mapumziko na kuwahakikishia ushindi Marekani.

Ni mara ya nne mtawalia kwa Marekani kufuzu kwa raundi ya mwondoano ya Kombe la Dunia.

Marekani wanaoongoza kundi D kwa alama sita wamejiunga na wenyeji wenza Mexico, ambayo ilikuwa timu ya kwanza kufuzu kwa raundi ya 32 bora.

Share This Article