Klabu ya Manchester City ya Uingereza imepatikana na hatia katika makosa 114 kati ya makosa yote 115 yaliyowalishwa kwa ukiukaji wa sheria za kifedha za Ligi Kuu Uingereza.
Hata hivyo adhabu ya Mancity bado haijabainika ingawa vlabu kadhaa vinapanga kuishtaki kwa hasara ya kifedha vilivyopata kwa kutoshiriki Ligi ya mabingwa Ulaya.
Baadhi ya adhabu ambazo huenda Mancity watapewa ni pamoja na kupokonywa alama na kupoteza mataji pamoja na kutimuliwa kutoka ligi Kuu.
Makosa hayo yalifanyika baina ya mwaka 2009 na 2018 na yalianza kuchunguzwa baada ya kuangaziwa na gazeti moja la Ujerumani.
Mancity hata hivyo waaminika kuwa tayari kukata rufaa dhidi ya uamuzi na adhabu zitakazotolewa.