Kenya Police Bullets FC kuchuana na Yei Joint Stars nusu fainali ya CECAFA

Police Bullets waliongoza kundi B baada ya kuwashinda Simba Queens ya Tanzania, mabao 2-1, katika mchuano wa ufunguzi kabla ya kuwanyuka Top Girls Academy 3-1.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa wa Ligi ya Kenya ,Police Bullets FC, watashuka uwanjani  Kigali Jumamosi jioni kwa mechi ya nusu fainali kuwania Kombe la CECAFA, dhidi ya Yei Joint Stars kutoka Sudan Kusini.

Police Bullets waliongoza kundi B baada ya kuwashinda Simba Queens ya Tanzania, mabao 2-1, katika mchuano wa ufunguzi kabla ya kuwanyuka Top Girls Academy ya Burundi 3-1 .

Yei Joint Stars iliongoza kundi A kwa pointi 6 .

 

Share This Article