Timu ya taifa ya soka ya Kenya-Harambee Stars imelazimishwa kutoka sare ya baoa moja na Eritrea, katika mchuano wa kundi D, kufuzu kwa fainal za mwaka ujao za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON).
Kenya inayofunzwa na benni McCarthy iloijipata nyuma katika dakika ya 36 kupitia kwa Nahom Girmai huku wageni wakiongoza kufikia mapumzikoni.
Harambee Stars ilikomboa bao hilo katika dakika za jioni kupitia kwa mshambulizi anayepiga soka ya kulipwa nchini Ubelgiji Ryan Ogam baada ya kupokea pasi ya Ben Stanley Omondi.
Stars watazuru Guinea wiki ijayo kwa mechi ya pili ya kundi hilo wakati Eritrea wakiwaalika Afrika Kusini.
Kenya inatumia mechi hizo kujiandaa kwa makala ya 36 ya fainali za AFCON kati ya Juni na Julai mwaka ujao .