Bingwa wa Afrika katika mbio za 800 Sarah Moraa na mshindi wa nsihani ya fedha ya Afrika katika mita 3000 kuruka viunzi na maji Edmund Serem ni miongoni mwa wanariadha 19, waliojumuishwa katika kikosi cha Kenya kitakachoshiriki mashindano ya Dunia kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka 20, nchini Peru mwezi Agosti mwaka huu.
Moraa ambaye alikosa tiketi ya Olimpiki mwaka huu, atashiriki mita 800 katika mashaindano ya Dunia pamoja Janet Jepkemoi .
Mercy Chepkemoi na Sheila Jebet watashiriki mashindano mawili kila mmoja , Chepkemoi akishiriki mita 3,000 na 5,000, huku Jebet akishiriki mita 1,500 na mita 5,000.
Hata hivyo wanariadha wa mbio za masafa mafupi walikosa kufuzu hatua iliyochangiwa na kuahirishwa kwa uteuzi huo kulingnana na kocha mkuu Robert Ng’isirei kutoka Julai hadi Juni.
Kikosi hicho kinatarajiwa kuripoti kambini mwezi ujao kujiandaa kwa makala ya 20, ya mashindano ya Dunia, yatakayoandaliwa mjili Lima Peru kati ya Agosti 27 na 31 mwaka huu.
Kenya ilimaliza ya nne katika makala ya mwaka 2022 mjini Cali, Colombia kwa dhahabu 3 fedha 3 na shaba 4.