Bingwa wa Afrika wa mita 800 maajuzi Sarah Moraa ni miongoni mwa wanariadha 200, wanaotarajiwa kushiriki marajiribio ya kitaifa uwanjani Nyayo kati ya leo na kesho.
Majaribio hayo ya chipukizi chini ya umri wa miaka 20,yatashuhudia chama cha riadha Kenya,kikiteua kikosi cha wanariadha takriban 36 watakaoshiriki mashindano ya Dunia mwezi Agosti mjini Lima Peru.
Kulingana na Mkurugeni wa riadha ya chipukizi katika chama cha Riadha Kenya,Barnaba Korir wanariadha wawili wa kwanza wataotimiza muda watafuzu watajumuishwa katika timu ya mashindano ya Dunia.
Punde baada ya uteuzi timu hiyo itaripoti katika kambi ya mazoezi kujiandaa kwa mashindano ya Dunia, yatayoandaliwa baina ya Agosti 27 na 31.
Kenya iliibuka ya nne mwaka 2022 mjini Cali Colombia kwa dhahabu 3 fedha 3 na shaba 4.