Serikali imetangaza kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa wa Mpox humu nchini.
Katibu katika Wizara ya Afya Mary Muthoni amesema mlipuko wa ugonjwa huo umeripotiwa kutokea kwenye mpaka wa Taita Taveta (OSBP) kutoka kwenye mtu mmoja aliyekuwa akisafiri kuelekea nchini Rwanda kutoka Uganda kupitia Kenya.
Mpox ni ugonjwa unaosbabishwa na virusi vya monkeypox.
Wanaoambukizwa ugonjwa huo hukumbwa na dalili kama vile homa, kichwa kuumwa, kutokwa na vipele.
Ugonjwa huo unaweza ukaambukizwa kupitia kugusa ngozi ya mtu aliyeambukizwa au vidonda kwenye mdomo au viungo vya uzazi.
Kufuatia mlipuko huo, Muthoni amewataka Wakenya kufuata hatua za afya ya umma ili kujilinda, kunawa mikono kwa maji kwa kutumia sabuni na kutafuta ushauri wa daktari ikiwa umeambukizwa.
Watu pia wametakiwa kuepuka kutangamana na watu wanaoshukiwa kuambukizwa ugonjwa huo.