Mkutano wa “Kujadiliana kwa Pamoja Fursa mpya kutokana na uchumi wa China” wa CGTN KISWAHILI wafanyika Nairobi

CGTN Kiswahili
9 Min Read

Mkutano wa “Kujadiliana kwa pamoja Fursa Mpya kutokana na Uchumi wa China” ulioandaliwa na Idhaa ya Kiswahili ya Kituo cha Kimataifa cha Televisheni cha China (CGTN) cha Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) umefanyika tarehe 6 mjini Nairobi, Kenya.

Mkutano huo uliwakutanisha wasomi, wawakilishi wa biashara, na maafisa kutoka maeneo maalum ya kiuchumi na maeneo ya usindikaji wa bidhaa za kuuza nje.

Katika mkutano huo, wataalamu wa masuala ya uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi wamechambua na kuelezea sera za maendeleo ya kiuchumi na kijamii zilizotolewa katika Ripoti ya Kazi ya Serikali ya Mikutano Mikuu Miwili ya Mwaka 2025.

Mkutano huo uliwashirikisha pia wakuu wa vyombo muhimu vya habari, wasomi na wanaviwanda nchini Kenya, na kuonesha ustahimilivu mkubwa na mustakabali mzuri wa uchumi wa China, kuingiza uhakika kwa ukuaji wa uchumi barani Afrika, na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa maendeleo na ustawi duniani.

Mkuu wa Kitengo cha Mambo ya Nje katika Chuo Kikuu cha Nairobi, ambaye pia ni mkurugenzi wa Kituo cha Masuala ya China na Afrika, Profesa Patrick Maluki, ametoa hotuba kuhusu ripoti ya kazi iliyotolewa kwenye Mikutano Mikuu Miwili ya China mwaka huu. Amesema, mikutano hiyo miwili ikiwa dirisha muhimu kwa dunia kuchunguza na kufahamu China, inafuatiliwa na watu wote duniani.

Profesa Maluki alisema China imeondoa vikwazo vya uagizaji wa bidhaa za kilimo, hatua inayowezesha parachichi, kahawa, na chai kutoka Afrika kuingia katika soko lake. Maonesho kama Maonesho ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika na Maonesho ya Kimataifa ya Uagizaji wa Bidhaa ya China (CIIE) yanatoa fursa kwa wafanyabiashara wa Afrika kupenya katika soko kubwa la China. Aidha, ripoti ya kazi ya China inasisitiza umuhimu wa digitali katika uchumi, ikitoa fursa kwa mataifa ya Afrika kuboresha mifumo yao ya kidijitali na kuimarisha biashara zao.

Profesa. Maluki amesema, Waziri Mkuu Li Qiang ameweka lengo la ukuaji wa Pato la Taifa la China la 5% kwa mwaka katika ripoti yake ya kazi ya serikali, ikizingatia kazi kuu ya maendeleo yenye sifa bora, na kuweka majukumu muhimu kama vile kujenga mfumo wa viwanda vya kisasa, kuongeza mahitaji ya ndani na kuhimiza mabadiliko ya uchumi ya kijani yenye kiwango cha chini cha utoaji wa kaboni.

Kama ilivyoonyeshwa katika ripoti hiyo, China inatarajiwa kudumisha ustahimilivu wa biashara ya nje kwa kupanua soko la mseto, na kuongeza sifa na thamani za nyongeza za bidhaa. Uwekezaji utaelekezwa kutokana na sera na kuzingatia uvumbuzi wa kisayansi, teknolojia na viwanda vya kijani, na kuwa injini mpya wa ukuaji wa uchumi.

Profesa Maluki ameeleza imani kubwa juu ya mustakabali wa maendeleo ya uchumi barani Afrika, akisema uchumi wa karibu asilimia 80 ya makundi ya kiuchumi ya Afrika unakua kwa asilimia 3.4. ambacho ni kiwango cha wastani duniani, na kwamba Afrika itaweza kujifunza kutokana na mfano mzuri wa China, akitolea mfano maeneo gani ambayo pande hizo za China na Afrika yanafanana, na masuala ambayo yanaweza kuboreshwa, mambo ambayo nchi za Afrika zinafuatilia wakati wa kujiendeleza.

Katika mkutano huo, wajumbe wa wafanyabiashara wa China na Kenya, wakuu wa vyombo vya habari, wataalam na wasomi wamefanya mazungumzo na majadiliano ya kina kuhusu fursa mpya zilizoletwa na maendeleo ya uchumi wa China kwa Afrika, na maendeleo ya ushirikiano kati ya China na Afrika katika sekta mbalimbali zikiwemo uwekezaji na nishati ya kijani. Wajumbe hao kwa kauli moja wameeleza imani yao thabiti kwa uhai na uthabiti wa uchumi wa China, na manufaa makubwa kwa Afrika.

Waziri wa Biashara, Viwanda, Utalii na Ubunifu wa Kaunti ya Machakos, John Kilonzo: China Ni Mshirika Muhimu wa Biashara wa Kenya

Waziri wa Biashara, Viwanda, Utalii na Ubunifu wa Kaunti ya Machakos, John Kilonzo, amesema China ni mmoja wa washirika wakuu wa kibiashara wa Kenya kutokana na uwezo wake mkubwa wa uzalishaji viwandani.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Biashara ya Kenya (KenTrade) mwaka 2023, China ilikuwa mshirika wa pili kwa ukubwa wa uagizaji wa bidhaa nchini Kenya kwa shilingi bilioni 110 na mshirika wa tisa wa uuzaji wa bidhaa nje shilingi bilioni 6.8.

Amesema Ili kuimarisha biashara ya usafirishaji bidhaa nje katika Kaunti ya Machakos, serikali inashirikiana na mashirika muhimu ya kitaifa, yakiwemo KenInvest, EPZA, SEZA, na mengineyo.

Meneja Mkuu wa Uhamasishaji Uwekezaji na Maendeleo ya Biashara katika Mamlaka ya Uwekezaji Kenya (KenInvest) Pius Rotich amesema kama kiashirio muhimu cha uchumi wa China, anafuatilia sana jinsi ripoti ya kazi ya serikali ya China ya mwaka huu itakayopangia kazi za kiuchumi, kwani ikiwa ni nchi ya pili kwa ukubwa wa uchumi mkubwa duniani, sera zinazotolewa kwenye mikutano miwili ya China zimevuka mipaka ya kitaifa. Amesema hivi sasa kuna takriban makampuni 3,000 ya China ambayo yamewekeza barani Afrika, hali ambayo inamaanisha fursa kubwa. Ameongeza kuwa Mamlaka ya Uwekezaji ya Kenya pia itafahamu vizuri zaidi fursa ya soko la China kupitia ripoti ya kazi ya serikali ya China.

Msomi maarufu wa masuala ya kimataifa wa Kenya Cavince Adhere ameeleza kuwa, kutokana na ripoti ya Makadirio ya Ukuaji wa Uchumi Duniani iliyotolewa hivi karibuni na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), uchumi wa Afrika, kusini mwa Jangwa la Sahara, utaongezeka hadi asilimia 4.2 mwaka 2025. Amesema mabadiliko ya dijitali, uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, mabadiliko ya nishati, na utandawazi wa kiuchumi wa kikanda vimekuwa msukumo muhimu wa maendeleo ya uchumi barani Afrika.

Ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya China na Afrika umeingia katika kipindi kipya cha kuongeza ubora, huku pande hizo mbili zikipanua ushirikiano mpya katika sekta za uchumi wa kijitali na mabadiliko ya nishati. Pia amesema, China inazisaidia nchi za Afrika kuendeleza nishati mbadala na kuboresha ujenzi wa miundo mbinu ya nishati ya umeme kwa kupitia kuhamisha teknolojia, ushirikiano na utoaji wa msaada wa fedha, mambo ambayo yanawafanya watu wa Afrika kufahamu zaidi faida zinazoletwa na ukuaji wa uchumi wa China na ushirikiano kati ya Afrika na China.

Mkuu wa Kituo cha Televisheni cha Embu nchini Kenya Grace Njenga, amepongeza mkutano huo, na kusema mwaka 2024, alitembelea mji wa Zhengzhou nchini China, na kushuhudia mafanikio ya China katika kuhifadhi na kurithi utamaduni wa jadi, kushughulikia mazingira ya Mto Huanghe, na kuendeleza sayansi na teknolojia. Ameongeza kuwa uchumi wa China una nguvu na uhai mkubwa, na China inazidi kupanua ufunguaji mlango wake wa hali ya juu, na nchi za Afrika zinatarajia kunufaika na maendeleo ya kasi ya China, ili kupata nguvu ya kujiendeleza.

Mhariri mkuu wa Kituo cha Televisheni ya Taifa cha Kenya, ambaye aliwahi kutembelea China na kuripoti habari za China, Martin Mwanje, ameelezea hisia zake aliporipoti mafanikio ya China katika ujenzi wa ikolojia. Kuhusu maoni ya China kwamba “Maji na milima ya kijani ni mali ya thamani”, amesema China imekamilisha sheria katika nyanja husika ikiwemo kushughulikia uchafuzi wa hewa, uchafuzi wa maji, na uchafuzi wa udongo, na kueneza mawazo ya kuhifadhi mazingira, uzoefu ambao unastahili kuigwa na nchi nyingine zinazoendelea.

Naibu mkuu wa Shirikisho la Wanafunzi wa Kenya waliosoma nchini China Joseph Maritim, amesema China inaongoza duniani katika nyanja nyingi za teknolojia za hali ya juu, haswa tangu mwaka huu, ambapo China imepiga hatua kubwa katika akili bandia, roboti zenye umbo la binadamu, magari ya umeme na nyanja nyinginezo, na kuendelea kufuatiliwa duniani. Ameongeza kuwa teknolojia hizo za kisasa pia ni fursa kubwa kwa Afrika, ambayo inataka kuzidisha ushirikiano na China katika kuunda kituo cha data, na kupata huduma za hesabu za mawingu, ili kutoachwa nyuma na zama mpya.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *