Mkurugenzi wa Secret Service nchini Marekani ajiuzulu

Tom Mathinji
1 Min Read
Mkurugenzi wa Secret Service Kimberly Cheatle, amejiuzulu

Siku chache baada ya shambulio la risasi dhidi ya Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, Mkurugenzi wa idara ya Secret Service Kimberly Cheatle, amejiuzulu.

Alipofika mbele ya kamati ya bunge siku ya Jumatatu, Cheatle alikiri kuwa Secret Service ilitepetea katika kuzuia shambulizi hilo dhidi ya Trump.

Matamshi hayo ya Cheatle kwamba idara yake ilishindwa kutoa ulinzi kwa Trump, yalisababisha vyama viwili vikuu vya kisiasa nchini Marekani kumshinikiza ajiuzulu.

Katika kikao hicho na wabunge, Cheatle hakuwaridhisha wabunge hao kuhusu jinsi shambulizi hilo lilitekelezwa, akisema uchunguzi unaendelea.

Mnamo Julai 13, mshambulizi Thomas Matthew Crooks mwenye umri wa miaka 20, alipaa juu ya nyumba na kumshambulia Trump alipokuwa akihutubia mkutano wa kisiasa mjini Butler, Pennsylvania.

Mshambuliaji huyo alimfyatulia risasi Trump kwa bunduki aina ya AR dakika chache baada ya Trump.

Hata hivyo mshambulizi huyo aliuawa kwa kupigwa risasi na afisa wa Secret Service chini ya sekunde 30 baada ya kufyatua risasi ya kwanza, kati ya nane zilizotumika.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *