Mkondo wa pili wa mbio za nyika nchini utaandaliwa kesho katika shule ya Kapsokwony Boys eneo la mlima Elgon.
Mbio hizo zitakuwa za vitengo vya kilomita 10 kwa wanaume na wanawake,kilomita 6 wasichana na kilomita 8 wanaume walio chini ya umri wa miaka 20 na kilomita 10 mseto kupokezana kijiti.
Mkondo wa Kapsokwony unafuata ule wa kwanza ulioandaliwa kaunti ya Machakos wiki jana.
Wanariadha walifika leo katika shule ya Kapsokwony Boys kujiandikisha na kuchukua nambari za tayari kwa mashindano ya kesho yatakayoandaliwa katika shule hiyo.
Washindi wa kilomita 10 watatuzwa shilingu 50,000 nafasi ya pili 40,000 na 30,000 kwa watakaomaliza nafasi za tatu.
Katika mbio za chipukuzi washindi watapokea shilingi 30,000,nafasi ya pili 20,000 na nambari tatu 15,000.
Mshindi wa mbio za kupokezana kijiti atabugia shilingi 10,000,nafasi ya pili shilingi 7,000, na shilingi 5,000 kwa watakaomaliza katika nafasi za tatu.