Gor Mahia wapigwa na butwaa na City Stars

Hansel Ochieng aliwaweka City Stars, uongozini kunako dakika ya nne kabla ya Benson Omalla, kuwasawazisha dakika sita baadaye.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa watetezi Gor Mahia, wamejipata njia panda baada ya kuambulia kichapo cha mabao 2-1 na Nairobi City Stars, katika uwanja wa Dandora kaunti ya Nairobi.

Hansel Ochieng aliwaweka City Stars, uongozini kunako dakika ya nne kabla ya Benson Omalla, kuwasawazisha dakika sita baadaye.

Vincent Owino alipachika bao la ushindi kwa wageni katika dakika ya 16 kupitia mkwaju wa penati.

Matokeo hayo yametia dosari harakati za Gor kuhifadhi ubingwa wa Ligi wakisalia alama 5 nyuma ya viongozi Police FC wakisalia na mechi 4 kuhitimisha msimu.

Katika pambano la awali uwanjani Dandora, KCB walizabwa bao moja kwa sifuri na Kariobangi Sharks.

Website |  + posts
Share This Article