Rais Ruto amewaahidi wachezaji wa timu ya taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars shilingi milioni 2.5 kila mmoja, endapo wataishinda Zambia Jumapili hii katika mechi ya mwisho ya kundi A kuwania kombe la CHAN.
Aidha, Ruto ameahidi kuwa endapo Kenya watashinda mechi ya robo fainali, kila mchezaji atapata nyumba ya vyumba viwili zilizo chini ya mpango wa nyumba za gharama nafuu mahali watakapochagua pamoja na kitita cha shilingi milioni 1 kila mmoja.
Ruto amesema haya leo alipozuru kambi ya timu hiyo katika mkahawa wa Pullman eneo la Upper Hill.
Ruto aliipongeza Harambee Stars kwa ushindi wao wa jana wa bao moja kwa bila dhidi ya Morocco na kuongoza kundi hilo kwa pointi 7.
Ameongeza kuwa ushindi wa Harambee Stars katika mechi za CHAN umewaunganisha Wakenya, akiwapa changamoto ya kujiamini na kushinda kombe hilo la CHAN.