Wanafunzi 9 kati ya 21 waliofariki katika mkasa wa moto uliotokea kwenye shule ya Hillside Endarasha Academy katika kaunti ya Nyeri wiki tatu zilizopita watazikwa leo Alhamisi.
Hii ni kulingana na Gavana wa kaunti ya Nyeri Mutahi Kahiga aliyezungumza wakati wa ibada ya wanafunzi hao iliyoandaliwa leo Alhamisi.
Kulingana na Gavana Kahiga, mazishi ya wanafunzi hao yataendelea hadi keshokutwa Jumamosi huku miili ya wanafunzi 10 ikipangiwa kuzikwa kesho Ijumaa.
Miili ya wanafunzi 2 itazikwa Jumamosi.
Ibada ya kuwaenzi wanafunzi hao ilifanyika leo Alhamisi katika uwanja wa Mweiga katika kaunti ya Nyeri.
Ibadi hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Rais Rigathi Gachagua na viongozi wa upinzani wakiongozwa na Kalonzo Musyoka.