Misri yawasilisha meli ya zana za kivita nchini Somalia

Dismas Otuke
1 Min Read

Meli ya kivita ya Misri imewsilisha shehena ya pili ya zana za vita mjini Mogadishu Somalia, hali inayoongeza mchecheto baina ya mataifa hayo mawili na Ethiopia.

Misri na Somalia wameongeza ukuruba wao mwaka huu kutokana na kukosa imani dhidi ya Ethiopia,hali ambayo imechangia Misri kutuma meli zaidi za zana za vita mjini Mogadishu, mwezi mmoja pekee tangu mataifa hayo mawili yatie saini mwafaka wa usalama.

Ethiopia ilitia msumari moto kwenye kidodonda Januari mwaka huu, iliposaini mkataba wa maelewano wa kukodi bahari yao eneo la Somaliland, ili iunge mkono kujitenga kwa Somaliland kutoka kwa Somalia.

Yamkini Misri imewaonya raia wake katika ubalozi wake mjini Mogadishu dhidi ya kusafiri kuelekea Somaliland kutokana na ukosefu wa usalama.

Ethiopia ina wanajeshi 3,000 walio katika kundi la usalama wa Muungano wa Afrika ambao wako nchini Somalia.

Website |  + posts
Share This Article