Mhubiri afungwa miaka 38 gerezani

Tom Mathinji
1 Min Read
Mhubiri Samuel Ngumbao Harrison.

Mhubiri  wa umri wa miaka 27 ambaye aliwadhulumu kimapenzi wanafunzi wawili wa shule ya msingi katika visa tofauti, amehukumiwa kifungo cha miaka 38 gerezani.

Katika kesi ya kwanza, hakimu mkazi wa Mariakani Olivia Koranje, alimhukumu Samuel Ngumbao Harrison miaka 30 gerezani kwa kumdhulumu kimapenzi mwanafunzi wa umri wa miaka 14.

Hakimu Koranje alidokeza kuwa hukumu dhidi ya Samuel iliambatana na sheria, baada ya mashahidi sita kutoa ushahidi wa kuaminika.

Katika kesi ya pili, hakimu mkuu wa Mariakani Nelly Adalo, alimhukumu Samuel kifungo cha miaka nane gerezani, kwa kumdhulumu kimapenzi mwanafunzi wa umri wa miaka 16.

Hakimu Adalo alitangaza kuwa upande wa mashtaka ukiongozwa na Jethron Okumu, ulithibitisha kuwa mshtakiwa alitekeleza uovu huo.

Samuel aliwadhulumu kimapenzi wanafunzi hao wawili tarehe 12 mwezi Agosti na tarehe 17 mwezi Agosti mwaka 2022, katika eneo la Mwavumbo kaunti ndogo ya Samburu, kaunti ya Kwale.

Wanafunzi hao walielezea jinsi mhubiri huyo alivyowahadaa waingie kwa nyumba kabla ya kuwadhulumu kimapenzi.

TAGGED:
Share This Article