Kampuni ya usambazaji umemenchini KPLC, imetangaza kukatiza kwa mfumo wake wa kununua umeme kabla ya matumizi kwa kipindi cha saa 24, ili kuwezesha uboreshaji wa huduma.
Wateja wamearifiwa kuwa mfumo huo utatatizwa kuanzia Jumapili Juni 2, saa 10 jioni na utarejelea hali ya kawaida Jumatatu Juni 3, saa 10 jioni.
Katika kipindi hiki, wateja hawataweza kununua umeme kutoka kwa vituo vyovyote vya kuuza vikiwemo afisi za Kampuni hiyo ya umeme KPLC, kwa njia ya simu M-Pesa na Airtel ikiwa ni pamoja na njia zote za benki.
KPLC imewahimiza wateja wote kununua umeme wa kutosha mapema ili kuepuka usumbufu wowote.