Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, alilazimika kukatiza ziara yake nchini Afrika Kusini, ghafla jana kufuatia mashambulizi ya Urusi, nchini mwake yaliyosababisha vifo vya watu tisa na kuwajeruhi wengine 70 .
Mashambulizi hayo ndiyo mabaya zaidi kuweza kutekelezwa nchini Ukraine, tangu Julai mwaka jana .
Zaidi ya droni 250 zilitekeleza mashambulizi hayo yaliyojumuisha kurushwa kwa makombora ya angani.
Ziara ya Zelensky nchini Afrika Kusini inafufua uhusiano wa mataifa hayo mawili baada ya ushirikiano kati ya mji wa Pretoria, kuwa na ushirikiano wa karibu na Rais wa Urusi Vladmir Putin.