Messi kuongoza Argentina kutetea Kombe la Dunia

Kocha Lionel Scaloni amemjumuisha Messi kwenye kikosi cha wanandinga 26, huku wakijumuishwa kundi J pamoja na Jordan,Austria na Algeria.

Dismas Otuke
1 Min Read

Lionel Messi atakuwa nahodha wa Mabingwa watetezi Argentina kwenye patashika ya Kombe la Dunia kati ya Juni 11 na Julai 19 mwaka huu katika mataifa ya Mexico, Marekani na Canada.

Kocha Lionel Scaloni amemjumuisha Messi kwenye kikosi cha wanandinga 26, huku wakijumuishwa kundi J pamoja na Jordan, Austria na Algeria.

Argentina italenga kuwa timu ya pili kutetea Kombe la Dunia tangu Brazil waafikie ufanisi huo mwaka 1962.

Hata hivyo, wachezaji tisa waliotwaa kombe hilo miaka minne iliyopita nchini Qatar wametemwa.

Wao ni Franco Armani, Juan Foyth, German Pezzella, Marcos Acuna, Angel Di Maria, Alejandro Gómez, Guido Rodriguez, Paulo Dybala, Angel Correa, na Franco Mastantuono.

Kikosi kamili

Makipa
Emiliano Martínez
Geronimo Rulli
Juan Musso

Madifenda
Nahuel Molina
Gonzalo Montiel
Cristian Romero
Leonardo Balerdi
Nicolas Otamendi
Lisandro Martinez
Nicolas Tagliafico
Facundo Medina

Wachezaji wa kiungo cha kati
Leandro Paredes
Alexis Mac Allister
Rodrigo De Paul
Giovanni Lo Celso
Exequiel Palacios
Enzo Fernandez
Valentin Barco

Washambulizi
Lionel Messi
Julian Alvarez
Lautaro Martinez
Thiago Almada
Nicolas Paz
Nicolas Gonzalez
Giuliano Simeone
Jose Manuel Lopez

Share This Article