Kenya ni ya tatu kuelekea siku ya mwisho ya mashindano ya Riadha Afrika

Nishani za fedha zilitwaliwa na Silvia Jerono na Stephen Ndagiri katika kilomita 20 matembezi.

Dismas Otuke
1 Min Read
Kevin Chesang (kulia) wakiwa na Silas Senchura, baada ya kunyakua dhahabu na shaba katika mita 10,000

Kenya inashikilia nafasi ya tatu kuelekea siku ya mwisho ya makala ya 24, ya mashindano ya riadha barani Afrika,jijini Accra,Ghana siku ya Jumapili.

Kenya imezoa jumla ya medali 10,dhahabu 4,fedha 2 na shaba 4, baada ya siku tano za mashindano.

Washindi wa dhahabu za Kenya ni:Diana Wanza na Kevin Chesang, katika mita 10,000,Kelvin Loti Kimtai, katika mita 800 na Edwin Too, katika shindano la Decathlon.

Nishani za fedha zilitwaliwa na Silvia Jerono na Stephen Ndagiri, katika kilomita 20 matembezi.

Walionyakua nishani za shaba kwa Kenya ni;Isaac Kimunu, katika urukaji mapana,Silas Senchura mita 10,000,Belinda Oburu, katika uruhsaji tufe na timu ya mita 400 kwa wanariadha wanne kupokezana kijiti jinsia mchanyato.

Share This Article