Comoros yasitisha kuongeza bei ya mafuta

Serikali ya Comoros iliongeza bei ya Dizeli kwa asilimia 46 na asilimia 35 kwa bei ya Petroli.

Dismas Otuke
1 Min Read

Comoros imetangaza kusitisha mpango wake wa kuongeza bei ya mafuta kufuatia maandano ya kitaifa kupinga ongezeko la bei ya mafuta.

Nchi hiyo ilitoa tangazo hilo Jumamosi iliyopita.

Hii inafuatia kuuawa kwa mtu mmoja na wengine watano kujeruhiwa vibaya wakati wa makabiliano baina ya polisi na waandamanaji.

Barabara zilifungwa wakati wa maandamano hayo ya Ijumaa kwa mawe kuendeleza mgomo wa kitaifa ulioanza nchini Comoros Jumatatu iliyopita.

Serikali ya Comoros iliongeza bei ya dizeli kwa asilimia 46 na petroli kwa asilimia 35.

Bei ya mafuta imeongezeka kote duniani kufuatia vita vinavyoendelea Mashariki ya Kati.

Wenye magari ya usafiri wa umma na wenye maduka walisambaratisha usafiri na shughuli za kawaida karibu na mji mkuu wa Moroni.

Mgomo huo na maandamano vililisitishwa Jumamosi baada ya serikali kusema haitaongeza bei ya mafuta ilivyokuwa imetangaza awali.

Share This Article