Timu ya taifa ya Kenya ya raga kwa wanaume saba upande maarufu kama Shujaa, itachauna na Ufaransa, leo katika mechi ya kuwania nafasi ya saba katika msururu wa pili wa Valladolid, nchini Uhispania siku ya Jumapili.
Kenya ambayo imeshinda mchuano mmoja pekee katika mkondo huo ilipoteza alama 21-0 dhidi ya Australia, katika robo fainali ya Kombe kuu Jumamosi usiku.
Katika hatua ya makundi Shujaa,ilishindwa alama 10-15, na Australia, katika kundi A kabla ya kunyukwa 0-14, na Afrika Kusini ,lakini wakagutuka na kuwabwaga Uingereza alama 12-7 katika mechi ya mwisho.
Shujaa ilimaliza ya saba katika mkondo wa kwanza wa Hongnkong na kujizolea pointi 8.