DCI yabaini wanafunzi saba walioteketeza shule ya Utumishi Academy

Kulingana na DCI washukiwa wanane waliokamatwa awali sita, walihusika na wako korokoroni huku mshukiwa mwingine akiachiliwa awali.

Dismas Otuke
1 Min Read
Bodi ya Usimamizi wa Utumishi Girls Academy yavunjwa.

Idara ya upepelezi wa kesi za jinai (DCI) imewatambua wanafunzi saba kati ya nane wanaokisiwa kuchoma shule ya Utumishi Girls Academy, katika kaunti ya Nakuru, na kusababisha vifo vya wenzao 16 wiki jana.

DCI imetumia ukanda wa CCTV kwa usaidizi wa Walimu kuwatambua saba hao wanaoamika kuwasha moto bweni hilo kabla ya kutoroka.

Kulingana na DCI washukiwa wanane waliokamatwa awali sita, walihusika na wako korokoroni huku mshukiwa mwingine akiachiliwa awali.

Haya yanajiri huku upasuaji ukikamilika katika makafani ya Hospitali ya Naivasha kwa mili 16 ya wanafunzi walioangamia.

Upasuaji huo ulioongozwa na mwanapatholojia Dkt Dorothy Njeri ulibaini kuwa wanafunzi hao 16 walifariki kutokana na kuchomeka.

Share This Article