Gor Mahia kutawazwa mabingwa leo huku msimu wa Ligi ukikamilika

Gor wanaongoza ligi ya Sportpesa kwa alama 69,pointi 5 zaidi ya AFC Leopards walio katika nafasi ya pili.

Dismas Otuke
1 Min Read

Gor Mahia FC watatawazwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Kenya, kwa mara ya 22 siku ya Jumapili ,baada ya mechi yao ya kufunga msimu dhidi ya Nairobi United FC katika uga wa Nyayo.

K’ogalo wametwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza tangu msimu wa mwaka 2023/2024,kabla ya kupokonywa taji na Police FC msimu jana.

Mechi zote za kufunga msimu zitachezwa sambamba kuanzia saa tisa alasiri.

Gor wanaongoza ligi ya Sportpesa kwa alama 69,pointi 5 zaidi ya AFC Leopards walio katika nafasi ya pili.

Ulinzi Stars,Mathare United na Kariobangi Sharks pia zitakuwa zikijaribu kuepuka  kuwa timu ya mwisho kuenguliwa ligini.

Mechi za Ligi raundi ya 34

Gor Mahia FC vs Nairobi United FC

Kariobangi Sharks vs Sofapaka

AFC Leopards SC vs Bidco United FC

Mathare United FC vs Bandari FC

Murang’a Seal FC vs Mara Sugar FC

Police FC vs Kakamega Homeboyz

Posta Rangers vs Ulinzi Stars

Shabana FC vs KCB FC

Tusker FC vs APS Bomet FC

Share This Article