Wanyonyi na Odira kutimka leo Rabat Diamond League

Wanyonyi ambaye pia ni bingwa wa Olimpiki atafungua msimu wake wa Diamond League, akilenga kurejesha taji hiyo aliyoshinda mwaka 2024, kabla ya kumaliza wa tatu mwaka uliopita.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa wa Dunia katika mbio za mita 800 Emmanuel Wanyonyi na Lillian Odira, watajitosa katika uwanja wa Mohammed VI, jijini Rabat, Morocco, kushiriki mkondo wa tatu wa mashindano ya Diamond League.

Wanyonyi ambaye pia ni bingwa wa Olimpiki atafungua msimu wake wa Diamond League, akilenga kurejesha taji hiyo aliyoshinda mwaka 2024, kabla ya kumaliza wa tatu mwaka uliopita.

Wanyonyi atakabiliana na Abdelaati El Guesse wa Morocco na Gabriel Tual wa Ufaransa pamoja na English Mark kutoka Ireland.

 

Odira naye atakuwa akishiriki mashindano ya Diamond League kwa mara ya kwanza katika amali yake ya Riadha.

Odira atapampana na mshindi wa mwaka jana Tsigie Duguma kutooka Ethiopia na Prudence Sekgodiso wa Afrika Kusini.

Mshindi wa nishani ya shaba ya Dunia Reynold Cheruiyot atatimka akipata upinzani mkali kutoka kwa Yared Nugusse wa Marekani.

Shindano jingine la Wakenya litakuwa mita 3,000 kuruka viunzi na maji wanaume,Edmund Serem,Simon Koech na Abraham Kibiwott, wakimenyana na bingwa wa Olimpiki mara mbili Soufiane El Bakkali wa Morocco.

Share This Article