Meneja wa zamani wa Uingereza Sven Goran Eriksson ameaga dunia Jumatatu akiwa na umri miaka 76.
Ni Januari mwaka huu ambapo Eriksson alifichua kuwa alikuwa amepatikana na saratani ya kongosho iliyokuwa imezagaa mwilini akiongeza kuwa hakuwa na zaidi ya mwaka mmoja wa kuishi.
Kifo cha Eriksson kimetangazwa na wakala wake Bo Gustavsson, aliyasema marehemu aliaga dunia akiwa amezingirwa na familia yake.
Marehemu amemwacha mpenziwe Yanisette, kakaze Lars-Erik na mkewe Jumnong, bintize Lina na mwanawe wa kiume Johan akiandamana na mkewe Amana na mkujukuu Sky.
Kocha huyo kutoka Uswidi alikuwa mkufunzi wa kwanza wa kigeni kuteuliwa kuiongoza timu ya taifa ya Uingereza mwaka 2001.
Mola ailaze roho yake mahali pema peponi.