Mchakato wa kumtafuta mwenyekiti mpya wa IEBC wang’oa nanga

Tom Mathinji
1 Min Read
Mchakato wa kumtafuta mwenyekiti wa IEBC umeanza Jumatatu.

Mahojiano ya kumtafuta mwenyekiti mpya wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), yameanza leo Jumatatu asubuhi huku wawaniaji 11 wakitarajiwa kufika mbele ya kamati ya uteuzi  katika Chuo cha Masuala ya Bima katika mtaa wa South C jijini Nairobi.

Mchakato huo unalenga kujaza nafasi iliyoachwa wazi baada ya muhula wa kuhudumu wa marehemu Wafula Chebukati kufika kikomo.

Wa kwanza kufika mbele ya kamati hiyo inayoongozwa na Dkt. Nelson Makanda alikuwa Abdulqadir Lorot Ramadhan.

Akihojiwa, Ramadhan alisema yuko tayari kutekeleza wajibu wake kwa uadilifu akielezea jinsi atakavyotumia tajiriba yake ya miaka 23 katika Idara ya Mahakama kuboresha utendakazi wake.

Msajili Mkuu wa zamani wa Idara ya Mahakama Anne Atieno Amadi, aliyekuwa Jaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki Charles Ayako Nyachae na Edward Katama Ngeywa pia wamepangiwa kufika mbele ya kamati hiyo leo Jumatatu.

Wale watakaosailiwa kesho Jumanne ni Erastus Edung Ethekon, Francis Kakai Kissinger, Jacob Ngwele Muvengeina Joy Brenda Masinde-Mdivo.

Nao wale watakaosailiwa siku ya Jumatano ni pamoja na Lilian Wanjiku Manegene, Robert Akumu Asembo Saul Simiyu Wasilwa.

Jumla ya watahiniwa 37 walikuwa wameonyesha nia ya kuwania nafasi ya uenyekiti wa IEBC kabla ya orodha hiyo kupunguzwa hadi watahiniwa 11.

Website |  + posts
Share This Article