McCarthy ateuliwa kocha wa Harambee Stars hadi mwaka 2027

Dismas Otuke
1 Min Read

Mshambulizi wa zamani wa Afrika Kusini Benni McCarthy, ameteuliwa kocha Mkuu wa Harambee Stars kwa mkataba wa miaka miwili.

McCarthy alizinduliwa Jumatatu jioni kwenye hafla ya kufana iliyoandaliwa jijini Nairobi na kuhudhuriwa na wadau wa soka nchini wakiongozwa na Rais wa shirikisho la soka nchini FKF Hussein Mohammed.

Kocha huyo mpya ameendamana na wasaidizi wake watatu: Vasili Manousakis ambaye ni naibu kocha, mkufunzi wa makipa Moneeb Josephs, na Pilela Maposa kama mtaalam wa takwimu za wachezaji.

Mkufunzi huyo aliye na umri wa miaka 47 ana leseni za UEFA B, A, na UEFA Pro, na amezinoa timu kadhaa zikiwemo Amazulu, Cape Town, na Sint Truiden akiwa naibu kocha, na mwisho alikuwa mkufunzi wa washamblizi katika kilabu ya Manchester United hadi mwaka uliopita.

Akizungumza baada ya kuzinduliwa, McCarthy amesema analenga kubuni kikosi thabiti na wasaidizi wake ili kuafikia matokeo bora.

Mtihani wa kwanza kwa McCarthy ni mechi ya kundi F kufuzu kwa fainali za kombe la dunia mwaka ujao dhidi ya Gabon baadaye mwezi huu katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo na Gambia.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *