Mbunge wa zamani wa Bomachoge Chache Simon Ogari afariki

Tom Mathinji
1 Min Read

Aliyekuwa mbunge wa Bomachoge Chache Simon Ogari ameaga dunia.

Viongozi wa kaunti ya Kisii wakiongozwa na Seneta Richard Onyonka na Seneta mteule Esther Okenyuri, walimuomboleza Ogari wakimtaja kuwa kiongozi shupavu na aliyejitolea kuwahudumia wakazi wa eneo hilo.

Seneta Onyonka, alimtaja mbunge huyo kuwa mnyenyekevu na aliyekuwa mkarimu.

Aidha, Onyonka alidokeza kuwa Ogari ambaye walihudumu pamoja katika bunge la 10 na 11, alijizatiti kuboresha maisha ya wakazi wa eneo bunge hilo, na mchango wake katika jamii utakumbukwa daima.

“Licha ya kuwa kiongozi bora, alikuwa urafiki wangu wa karibu Kwa muda wa miaka mingi,” alisema Onyonka.

“Utendakazi wake kwa watu wa Bomachoge utasalia kuwa kielelezo cha kupigiwa mfano.”

Share This Article