Mbunge wa Wajir Kaskazini alaani mauaji ya watu wawili

Tom Mathinji
2 Min Read
Mbunge wa Wajir Kaskazini Ibrahim Abdi Saney.

Mbunge wa Wajir Kaskazini Ibrahim Abdi Saney, amelaani vikali utekaji nyara na mauaji ya wakazi wawili wa eneo bunge hilo, yaliyotekelezwa na watu wanaodaiwa kuwa maafisa wa polisi.

Kulingana na mbunge huyo, Ahmed Omar Mohamed na Mohamed Ali Mohamed, walitekwa nyara Agosti 20, 2024, walipokuwa wakiendesha baiskeli katika mji wa Bute.

Maafisa hao wanadaiwa kuwateka nyara Issa Bulle Mohamed katika kituo cha kibiashara cha  Ajawa mnamo Agosti 22, 2024 huku Dadow Adow Mohamed (nambari ya kitambulisho 3329771) akiuawa kikatili.

Mbunge huyo alisema familia za waliotekwa nyara hadi sasa hazijui waliko wapendwa wao.

“Wasiwasi wangu ni je, tulifutilia mbali katiba lini na mfumo wetu wa sheria?. Ikiwa watu hao ni wahalifu ningependa kuona wamefikishwa mahakamani kufunguliwa mashtaka kupitia mchakato faafu na iwapo watapatikana na hatia wahukumiwe. Hatuna tatizo na hilo,” alisema Saney.

Saney alitoa wito kwa serikali kuwaachilia watu hao, na kuwajibikia mauaji ya mtu mmoja yanayodaiwa kutekelezwa na polisi.

“Maafisa wa polisi waliovalia mavazi ya raia wamekuwa wakipiga doria katika eneo bunge langu kwa muda wa wiki moja iliyopita wakitumia magari matatu, na wao ndio wamehusika na visa hivyo vya uhalifu,” alisema mbunge huyo katika mkutano na wanahabari leo Ijumaa katika majengo ya bunge.

‘Je, kila mshukiwa anapaswa kuuawa? Ni kipi kitasalia hapa nchini iwapo kanuni kwamba mtu atasalia bila

“Should every suspect be killed?  Mbona wakazi wa eneo bunge langu wauawe?. Ningependelea iwapo wangefunguliwa mashtaka na kuhukumiwa kulingana na ushahidi ambao ungetolewa,” alishangaa mbunge huyo.

Wakati huo huo mbunge huyo alielezea wasiwasi wake kuhusu hatua ya serikali ya kuwapokonya silaha maafisa wa polisi wa akiba katika eneo la kaskazini mwa nchini, huku bunduki 395 zikikusanywa katika kaunti ya Wajir pekee. 

“Maafisa hawa ndio wamekuwa wakikabiliana na kundi la Al Shabaab na makundi mengine ya kigaidi. Sasa maafisa hao wamepokonywa silaha,” alisema Saney.

Aliitaka serikali kubadili mfuo wake na kukoma kuwateka nyara na kuwatesa wakenya.

Share This Article