Ndege zisizo na rubani zashambulia Moscow

Tom Mathinji and BBC
1 Min Read
Moscow yashambuliwa na ndege zisizokuwa na rubani.

Mtu mmoja amedaiwa kuuawa, huku watatu kujeruhiwa baada ya ndege zisizokuwa na rubani kushambulia jiji la Moscow usiku kucha , kulingana na maafisa nchini Urusi.

Kulingana na wizara ya Ulinzi nchini Urusi, jumla ya ndege 337 za Ukraine zilizuiwa au kuharibiwa usiku kucha katika mkoa wa Moscow na mikoa mingine tisa ya Urusi.

Mashambulizi hayo yanajiri  saa chache kabla ya mkutano uliopangwa kati ya maafisa wa Marekani na Ukraine leo Jumanne kufuatia mzozo wa hivi majuzi kati ya Rais Trump na Rais Zelensky katika Ikulu ya White House.

Hili linaonekana kuwa shambulio kubwa zaidi la ndege zisizo na rubani ambazo Ukraine imeanzisha hadi sasa ndani na karibu na Moscow. Inahusisha kadhaa ya drones, baadhi yao kulenga maeneo ya makazi.

Viwanja vinne vya ndege vya Moscow vimelazimika kufungwa kwa muda.

Meya wa Moscow anasema ulinzi wa anga wa Urusi ulidungua zaidi ya ndege 60 zisizo na rubani walipokuwa wakikaribia mji mkuu.

Hata hivyo, Ukraine haijatamka lolote kuhusu mashambulizi hayo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *