Mbunge wa Naivasha Jayne Kihara aachiliwa kwa dhamana

Tom Mathinji
1 Min Read

Mbunge wa Naivasha Jayne Kihara ameachiliwa kwa dhamana ya kibinafsi ya shilingi 50,000.

Kihara alikuwa ameshtakiwa kwa kosa la kuvuruga amani kinyume cha sehemu ya 94 (1) ya katiba ya Kenya.

Hakimu Benmark Ekhubi, alimwachilia Kihara huku kesi ikisubiriwa ikiwa atashtakiwa dhidi ya kuvuruga amani.

Kesi hiyo dhidi ya Kihara itasikizwa Julai  29, 2025.

Kihara alifikishwa mahakamani siku moja baada ya kukamatwa na maafisa wa Idara Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) jana Alhamisi.

Hii ni baada ya kukaidi agizo la idara hiyo la kumtaka afike kwenye afisi zake kuandikisha taarifa akilitaja kuwa kinyume cha sheria.

Kihara alikamatwa kutoka nyumbani kwake Maraigushu na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Naivasha.

Kisha alishtakiwa kwa kuchochea ghasia zilizosababisha wafafanya biashara kupoteza mali.

Website |  + posts
Share This Article