Mbunge Peter Salasya atakiwa kuomba msamaha

Tom Mathinji
1 Min Read

Wawakilishi wadi wa bunge la kaunti ya Kakamega, wanashinikiza mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya kuomba msamaha.

Wawakilishi wadi hao wakiongozwa na spika James Namantsi aidha wanataka kupewa ulinzi.

Wakizungumza nje ya bunge la kaunti hiyo, viongozi hao walielezea kutamaushwa kwao na mienendo ya mbunge huyo na kutoa wito kwa spika wa bunge la kitaifa Moses Wetangula kuingilia kati.

Aidha wawakilishi wadi hao wanamtaka mbunge huyo kujirekebisha na kuheshimu viongozi wengine.

Wafuasi wa mbunge huyo hata hivyo walimtaka gavana wa Kakamega Fernandes Baraza kuandaa mkutano na viongozi wote waliochaguliwa katika kaunti hiyo, ili kutafuta suluhu kwa uhasama unaoendela kukidhiri baina ya wawakilishi wadi na wabunge.

Share This Article