Mbunge Baya aanzisha kampeini ya siku 10 kupinga matumizi ya Muguka Kilifi

Dismas Otuke
1 Min Read

Mbunge wa Kilifi kaskazini Owen Baya, ameanzisha kampeini ya siku 10 kupinga uuzaji na matumizi ya Muguka katika kaunti ya Kilifi.

Baya anesema ataendelea na kampeini hiyo licha ya kutishiwa kung’atuliwa wadhfa wake wa naibu wa walio wengi bungeni .

Baya amesema anataka kushinikiza upigaji marufuku ya matumizi ya zao hilo, ambalo limesambaratisha mausha ya vijana wengi.

Kilele cha maadhimisho ya siku hizo kumi ni tarehe 26 huu, ambayo ni siku ya kimataifa dhidi ya ulanguzi wa dawa haramu na mihadarati.

Viongozi kutoka kaunti hiyo akiwemo mwakilishi wa akina mama Gertrude Mbeyu na Waziri Jinsia Aisha Jumwa, wamekuwa kwenye mstari wa mbele kupinga matumizi ya zao hilo.

Makundi kadhaa ya wanawake pia yamepanga kuandaa maandamano ya kupinga matumizi ya Muguka.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *