Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino mapema leo Ijumaa alifikishwa katika mahakama ya Milimani kujibu mashtaka ya kushiriki maandamano.
Owino alikamatwa Jumanne wiki hii usiku katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, JKIA baada ya kuwasili kutoka Mombasa na kufungiwa katika korokoro ya Wang’uru kaunti ya Kirinyaga kabla ya kusafirishwa hadi Nairobi jana Alhamisi.
Mbunge huyo alifikishwa kizimbani chini ya ulinzi mkali wa maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Jinai, DCI na kukanusha mashtaka yote dhidi yake.
Baadaye, aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu 100 pesa taslimu au dhamana ya shilingi laki 2.
Haya yanajiri huku maandano ya upinzani dhidi ya serikali kulalamikia gharama ya juu ya maisha na matozo mapya yakiingia siku ya tatu.