Mawaziri wapya watatu walioteuliwa kusailiwa Jumanne

Mawaziri hao wateule ni Mutahi Kagwe (Kilimo), William Kabogo (Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali) na Lee Kinyanjui (Biashara).

Martin Mwanje
1 Min Read
Mutahi Kagwe - Waziri Mteule wa Kilimo

Mawaziri wapya watatu walioteuliwa kusailiwa Jumanne

Mawaziri wapya watatu walioteuliwa na Rais William Ruto katika mabadiliko yake ya hivi punde ya Baraza la Mawaziri watasailiwa kesho Jumanne. 

Wao ni aliyekuwa Waziri wa Afya Mutahi Kagwe na Magavana wa zamani William Kabogo wa Kiambu na Lee Kinyanjui wa Nakuru.

Kagwe ameteuliwa kumrithi Dkt. Andrew Karanja kama Waziri wa Kilimo huku Kabogo akiteuliwa kuchukua mahali pa Dkt. Margaret Ndung’u aliyekuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali.

Hata hivyo, Dkt. Ndung’u aliyekuwa ameteuliwa kuwa Balozi wa Kenya nchini Ghana amekataa uteuzi huo kutokana na sababu za kibinafsi.

Dkt. Karanja ameridhia uteuzi wake na tayari amesailiwa na ikiwa uteuzi wake utaidhinishwa na bunge, basi ataelekea nchini Brazil kuhudumu kama Balozi wa Kenya nchini humo.

Kwa upande mwingine, Kinyanjui ameteuliwa kuwa Waziri wa Biashara kuchukua mahali pa Salim Mvurya aliyekabidhiwa mikoba ya kuongoza Wizara ya Michezo.

Watatu hao watapigwa msasa na Kamati ya Bunge la Kitaifa juu ya Uteuzi katika zoezi litakaloendeshwa katika majengo ya bunge kuanzia kesho Jumanne asubuhi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *