Mawaziri wa nchi wanachama wa IGAD wakongamana Djibouti

Kenya inawakilishwa kwenye mkutano huo na Katibu katika Wizara ya Mambo ya Nje, Korir Sing’Oei.

Tom Mathinji
1 Min Read
Mawaziri wa nchi wanachama wa IGAD wakongamana Djibouti.

Mawaziri kutoka nchi wanachama wa shirika la kimaendeleo la IGAD, wanakutana kwenye mkutano 74 usio wa kawaida nchini Djibouti.

Mawaziri wa Mambo ya Nje na wawakilishi wao, wanatarajiwa kujadili kuhusu mambo muhimu ya kikanda kuhusu amani, usalama, masuala ya kitaasisi, huku wakielezea kujitolea kwao kufanikisha ushirikiano wa kanda hii.

Kenya inawakilishwa kwenye mkutano huo na Katibu katika Wizara ya Mambo ya Nje, Korir Sing’Oei.

Mkutano huo unatoa fursa kwa nchi wanachama kuchunguza hatua zilizopigwa kuleta amani na maendeleo ya kiusalama, juhudi za kikanda za kufanikisha udhabiti,na ushirikiano miongoni mwa mataifa yaliyo katika kanda ya IGAD.

Aidha, mkutano huo pia utajadili kuhusu utekelezaji na kuimarisha makubaliano ya IGAD, katika kuunga mkono majukumu ya shirika hilo na masuala muhimu ya kikanda.

Share This Article