Ripoti za hivi punde zinaashiria kwamba mwanamuziki wa muda mrefu wa Bongo Fleva toka nchini Tanzania Sefu Shabani Ramadhan maarufu kama Matonya ameomba usaidizi kutoka kwa mwanamuziki mwenza Diamond Platnumz.
Matonya amezuiliwa nchini Kenya huko Mombasa baada yake kushtakiwa kwa makosa ya ubakaji lakini mahakama ilimwachilia kwa dhamana ya shilingi laki 5 za Kenya, huku kesi yake ikiendelea lakini anaonekana kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Kulingana na ndugu yake kwa jina Omary ambaye yuko Kenya kwa ajili ya kumshughulikia usaidizi umekosekana kabisa na kwamba amepokonywa simu na hawezi kuwasiliana na yeyote.
Ni katika mahojiano na wanahabari ambapo alitoa wito kwa Diamond Platnumz akisema, “Nimepokonywa simu, sina mawasiliano na mtu yoyote, Lakini nina imani kubwa kuwa mdogo wangu Diamond Platnumz angeweza kunisaidia.”
Alielezea kwamba iwapo angepata namba ya Diamond, yeye ndiye anamtumainia pakubwa lakini tatizo ni namna ya kumfikia.
Matonya ambaye ni msanii wa Bongo Flava kwa zaidi ya miaka 15, anayefahamika kwa nyimbo kama “Vaileti” na “Anita” alishtakiwa kwa kile kinachosemekana kuwa unyanyasaji wa kingono.
Alifikishwa mahakamani Mombasa kuhusiana na kisa kilichotokea Aprili 7, 2026 huko Nyali, ambapo alikanusha mashtaka yote dhidi yake.
Kesi hiyo nashughulikiwa kwa mujibu wa sheria ya Kenya ya kukabiliana na makosa ya kingono ambapo mahakama ilimwachilia kwa dhamana yenye masharti makal yanayojumuisha kutosafiri kesi inapokuwa ikiendelea.