Matokeo ya KPSEA kutolewa kesho

Huo ndio mtihani wa kwanza wa kitaifa wa utathmini wa mtaala mpya CBC wa gredi ya 6 na ulifanyika kati ya Oktoba 28 na 30 mwaka 2024.

Marion Bosire
1 Min Read
Julius Ogamba - Waziri wa Elimu

Wizara ya elimu imetangaza kwamba baraza la mitihani ya kitaifa KNEC litatangaza matokeo ya mtihani wa gredi ya 6 KPSEA kesho Jumatatu Januari 6, 2025.

Ikumbukwe kwamba huo ndio mtihani wa kwanza wa kitaifa wa utathmini wa mtaala mpya CBC wa gredi ya 6 na ulifanyika kati ya Oktoba 28 na 30 mwaka 2024.

Wanafunzi 1,313,913 walifanya mtihani huo ambao una sehemu mbili moja ikiwa tathmini ya malezi na ya pili ikiwa tathmini ya kifupi ya ufahamu wa wanafunzi.

Sehemu ya kwanza ni katika kiwango cha shule na inawakilisha asilimia 60 ya matokeo jumla huku sehemu ya pili ikiwa ni ya kitaifa na inawakilisha asilimia 40 ya matokeo jumla.

Majibu ya KPSEA yatatumiwa pia kuafikia majibu ya mwisho kabisa ya mwanafunzi atakapokuwa akikamilisha sekondari msingi au Junior Secondary katika gredi ya 9.

Tangazo la wizara ya elimu linajiri siku chache baada ya waziri wa elimu Julius Ogamba kutangaza kwamba matokeo ya mtihani wa kidato cha nne KCSE mwaka 2024 yatatangazwa hivi karibuni.

Kulingana naye, kazi inayoendelea ni ya kutathmini matokeo hayo kabla ya kuyatangaza rasmi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *