Mateka wa Israel walidhulumiwa kingono

BBC
By
BBC
1 Min Read

Raia wa Israel ambao walitekwa nyara na Hamas na kupelekwa Gaza walipewa madawa za kulevya ili kuwafanya wawe watulivu na wengine kudhulumiwa kingono, kulingana na daktari anayewatibu baadhi ya wale ambao wameachiliwa.

Renana Eitan, mkurugenzi wa kitengo cha magonjwa ya akili katika Kituo cha Matibabu cha Tel Aviv Sourasky-Ichilov, alisema “unyanyasaji wa kimwili, kingono, kiakili, na kisaikolojia wa mateka hawa walioachiwa huru ni mbaya sana”.

“Sijawahi kuona kitu kama hicho” katika miaka 20 ya kuwahudumia waathiriwa wa kiwewe, alisema. ”

Mmoja wa wasichana alipewa ketamine kwa wiki chache,” aliongeza. ”

Watoto walitenganishwa na familia zao, na mgonjwa mmoja alimwambia Eitan kwamba mateka kadhaa walikuwa wamezuiliwa kwenye giza kwa zaidi ya siku nne.

“Walikuwa na akili, walikuwa na ndoto,” Eitan aliongeza.

BBC
+ posts
TAGGED:
Share This Article