Mashindano ya michezo kwa wanafunzi walemavu yazinduliwa

Michezo hiyo ya ukanda wa Magharibi ya nchi imeanzishwa hii leo katika uwanja wa Nalondo kwenye eneo Bunge la Kabuchai katika kaunti ya Bungoma

KBC Digital
1 Min Read

Michuano ya shule za upili ya wanafunzi wenye changamaoto za kimaumbile ukanda wa Magharibi ya Nchi imeanzishwa hii leo katika uwanja wa Nalondo kwenye eneo Bunge la Kabuchai katika kaunti ya Bungoma.

Michuano hiyo ni fursa kwa kiteuliwa kaa wanafunzi watakaowakilisha eneo la Magharibi kwa michuano ya kitaifa itakayoandaliwa katika kaunti ya Mombasa.

Mwenyekiti wa michezo hiyo Magharibi ya nchi Walter Kwanusu anasema kuwa Riadha hizo ni nafasi bora ya usawa nchini kwa watoto akiwataka wazazi kutoficha wanao na kukumbatia Elimu huku akitoa wito kwa wafadhili kuingilia kati na kuwapa msaada.

Ni kauli ambayo iliungwa mkono na Mkurugenzi wa Elimu Kaunti ya Bungoma Pius Ng’oma ambaye amesistiza kuwa ulemavu sio kikwazo akihimiza nidhamu na uwazi kwenye uteuzi wa watakaowakilisha eneo hilo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *