Mashindano ya Absa Sirikwa Classic mwaka 2025 yalifana

Dismas Otuke
1 Min Read

Makala ya nne ya mashindano ya Absa Sirikwa Classic World Cross Country, yaliyoandaliwa Jumamosi iliyopita ya eneo la Lobo Village jijini Eldoret, yalikuwa ya kufana na ya hadhi ya kimataifa.

Kutoka kwa maandalizi, haiba ya wanariadha walioshiriki kutoka humu nchini na kimataifa, idadi kubwa ya wanahabari waliohusika pamoja na idadi kubwa ya mashabiki waliojitokeza kuwashangilia wanariadha, ulilikuwa ushahidi tosha wa mashindano ya haiba kuu.

Zaidi ya wanariadha 1,000 kutoka nchi 40 tofauti walishiriki katika mashindano hayo, ikiwemo kutoka Uganda, Ethiopia, Poland, Ukraine, Jamhuri ya Czech, na wenyeji Kenya walishiriki katika vitengo sita tofauti vya mashindano bila kusahau mashindano ya watoto kati ya umri wa miaka 6 na 15.

Wafanyibiashara pia walivuna pakubwa kutoka kwa wachuuzi wa vyakula hadi wanabodaboda walifurika Lobo Village kuzumbua riziki wakati wa mashindano hayo.

Pongezi kwa kamati ya andalizi ya mashindano hayo ikiongozwa na Mkurugenzi wa mashindano hayo Barnaba Korir, mkurugenzi wa kiufundi wa mashindano Kennedy Tanui, mwenyekiti wa kamati andalizi ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha riadha eneo la Central Rift Abraham Mutai, ambao walihakikisha kila kitu kiko shwari.

Daniel Simiu na Agnes Jebet Ng’etich walishinda mbio za kilomita 10 kwa wanaume na wanawake mtawalia

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *