Mashabiki wa mwanamuziki wa Marekani Lil Durk wameandamana nchini Ghana wakitaka aachiliwe huru.
Wakiwa wamevaa shati tao zenye maandishi “Only The Family” ambalo ni jina la kampuni ya Durk ya muziki, mashabiki hao walitembea kwenye barabara za Ghana wakitaka aachiliwe.
Durk alikamatwa kwa tuhuma za kukodi watu kutekeleza mauaji mpango ambao unasemekana kuhusisha wanamuziki watano wa kampuni ya “Only The Family” mwaka 2022.
Wanamuziki hao Kavon Grant, Deandre Wilson, Keith Jones, David Lindsey na Asa Houston, walikamatwa Oktoba 23, 2024 kwa makosa yanayohusiana na mauaji hayo.
Inaripotiwa kwamba Durk aliwalipa wakampiga risasi binamu ya Quando Rondo kwa jina Lul Pab huko Los Angeles.
Lengo la Lil Durk lilikuwa kulipiza kisasi kwa mwanamuziki mwenza Quando Rondo, baada ya rafiki ya Quando kumfyatulia risasi na kumuua mwanamuziki King Von huko Atlanta.
Durk alikamatwa Oktoba 24, 2024 katika jimbo la Broward huko Florida kwa madai hayo ya kukodi wenzake kutekeleza mauaji.
Anapangiwa kuhamishiwa California ambako kesi dhidi yake itasikilizwa na kuamuliwa. Iwapo atapatikana na hatia, Durk ambaye amenyimwa dhamana, anakabiliwa na hukumu ya kifo.