Mashabiki wa klabu ya Arsenal nchini Kenya siku ya Jumapili wametembelea kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu hayati Raila Odinga nyumbani kwake Kang’o ka Jaramogi.
Mashabiki hao, wanaume kwa wanawake waliovalia jezi za klabu ya Arsenal, waliweka maua kwenye kaburi la Odinga, ambaye pia alikuwa shabiki mkuu wa Arsenal.
Raila alizikwa Jumapili iliyopita baada ya kufariki akiwa na umri wa miaka 80 akipokea matibabu nchini India.