Rais William Ruto amebatlisha marufuku ya kaunti za Mombasa na Kilifi, dhidi uuzaji na matumizi ya Muguka akisema kuwa kinyume cha katiba kwa hatua hiyo iliyochukuliwa.
Ruto alisema haya Jumatatu usiku alipokutana na viongozi wa kaunti ya Embu katika Ikulu ,akisisitiza kuwa kulingana na sheria za mwaka 2023,Muguka inatambulika kama mmea na wala sio kileo.
Kaunti ya Mombasa ilikuwa ya kwanz kupiga marufuku kuingizwa na kuuzwa kwa Muguka, ikifuatwa na kaunti ya Kilifi.
Viongozi wa kaunti hizo wamekuwa wakilalama kuhusu athari kubwa za Muguka kwa vijana wengi na pia wazee,huku ikichangia uzembe na kupunguza utendakazi.