Kiungo mkabaji mstaafu wa Kenya MacDonald Mariga ndiye mwaniaji mwenza wa Hussein Mohammed, kwenye uchaguzi wa shirikisho la soka nchini FKF unaoatarajiwa kuandaliwa Disemba 7 mwaka huu.
Kiungo mkabaji mstaafu wa Kenya MacDonald Mariga ndiye mwaniaji mwenza wa Hussein Mohammed, kwenye uchaguzi wa shirikisho la soka nchini FKF unaoatarajiwa kuandaliwa Disemba 7 mwaka huu.
Mariga aliye na umri wa miaka 37 alizinduliwa rasmi Ijumaa usiku katika kaunti ya Nairobi.
Kiungo huyo wa zamani ana tajriba pana ya soka baada ya kuichezea Harambee Stars mechi 40, na kufunga mabao matano kati ya mwaka 2003 na 2018.
Hussein Mohammed alikuwa mwaniaji wa kwanza kutangaza azma ya kuwania Uenyekiti wa FKF.
Baadhi ya ruwaza za Hussein na Mariga katika uaniaji Urais ni kuimarisha soka kuanzia mashinani,kuboresha soka ya vipusa na kuinua hadhi ya ligi zote pamoja kuinua maslahi ya wachezaji.
Uchaguzi wa FKF ngazi ya kaunti utaandaliwa Novemba 2 mwaka huu ukifuatwa na ule wa kitaifa Disemba 7.