Marekani imeanza kutuma silaha na zana za kijeshi kwa Israel na inahamisha meli za kivita za jeshi la wanamaji na ndege za kivita, katika eneo hilo ili kuonyesha inaunga mkono Israel.
Meli hizo tayari zilikuwa katika Bahari ya Mediterania, kwa hiyo hazikuwa na safari ndefu ya Kwenda Israel. Na sio kawaida kwa Amerika kupeleka meli za wanamaji katika eneo hilo wakati kuna milipuko.
Haijafanya hivyo wakati wa vita vya awali kati ya Hamas na Israel, ambayo yamekuwa ya kujitegemea. Lakini hii sio kuhusu Hamas. Pentagon ina wasiwasi kwamba mzozo unaweza kuenea.
Afisa mkuu wa ulinzi alisema meli hizo za kivita na ndege zimekusudiwa kuonyesha dhamira thabiti kwa ulinzi wa Israel, na kuizuia nchi yoyote au kundi la wanamgambo kujiunga na vita.
Hatua hiyo inailenga hasaa Iran, ambayo inaunga mkono vuguvugu lenye nguvu la Hizbollah la Lebanon, pamoja na Hamas.
Marekani itakuwa sehemu ya jibu la muda mrefu na lla kuiadhibu la Israel, ingawa msemaji wa Baraza la Usalama la Taifa John Kirby alisema hakuna nia ya kuweka jeshi la Marekani nkatika ardhi ya Israel.