Marekani, Misri na Qatar zatoa wito kwa Israel na Hamas kuanza tena mazungumzo

Martin Mwanje
1 Min Read

Marekani, Misri na Qatar zimetoa taarifa ya pamoja zikitaka Israel na Hamas kuanza tena mazungumzo kuhusu makubaliano ya kusitisha mapigano na kuachiliwa huru kwa mateka.

Taarifa hiyo ilisema mataifa hayo matatu yalitengeneza “mkataba wa mfumo” ambao “ni maelezo ya utekelezwaji yaliyoachwa kukamilishwa”.

Israel ilisema itatuma wapatanishi kwenye mazungumzo hayo yaliyopangwa kusainiwa tarehe 15 Agosti mjini Doha au Cairo. Hamas hawakujibu mara moja.

Msukumo huo mpya wa kidiplomasia utaonekana kama jaribio la kuzuia mivutano ya kikanda kuwa katika hali ya kushindwa kudhibitiwa, baada ya kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh kuuawa wiki iliyopita.

Huku Iran ikiilaumu Israel kuhusika na mauaji hayo, imeapa kujibu – ingawa Israel haijatoa maoni moja kwa moja kuhusu mauaji hayo.

Share This Article